Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan wanaitaka timu ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) kuleta ushindi wa heshima katika mechi ya marudiano dhidi ya timu ya Cameroon ya kufuzu mashindano ya soka ya dunia kwa kuibamiza mabao mengi kuliko ushindi wa mabao manne kwa nunge uliopatikana kwenye mechi ya awali Mei 22, 2022 nchini Cameroon. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo alipoitembelea timu hiyo akiambata na Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Michezo nchini pamoja na Viongozi Wakuu wa Shirikisho la soka Tanzania na Zanzibar kwenye uwanja wa Amani uliopo Zanzibar ambapo amefafanua kuwa watanzania wanaimani kubwa na timu hiyo ili kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kufungua milango ya Tanzania kuingia...